in

Kampuni ya Blackberry Yasitisha Kutengeneza Simu Zake

Hatimaye kampuni ya blackberry imeamua kuachana na utengenezaji wa smartphone zake

Kampuni ya Blackberry ambayo hapo awali ilikua maarufu sana kwa utengenezaji wa smartphone zenye ulinzi bora, hivi karibuni imetangaza rasmi kuachana na utengenezaji wa simu zake hizo.

Kampuni hiyo imetangaza kuwa baada ya kutengeneza simu zake mpya zenye kutumia mfumo wa uendeshaji wa Android kampuni hiyo ilijiwekea malengo ambayo kwa bahati mbaya hayakuweza kutimia hivyo kampuni hiyo ilipata hasara kubwa karibia dollar za kimarekani $372 million. Kutokana na hasara hiyo pamoja na mambo mengine mengi  ya kiuchumi bila shaka ndio sababu ya kampuni hiyo kuamua rasmi kuachana na utengenezaji wa simu zake yenyewe. Hata hivyo ripoti zinasema kuwa jina la Blackberry halita kufa bali kampuni nyingine itaendelea na uzalishaji wa simu hizo.

Habari kutoka kwenye tovuti mbalimbali zinasema kuwa kampuni hiyo imeamua kujikita zaidi kwenye uzalishaji wa vifaa vya ulizi, kwani wote tunajua kuwa kampuni hiyo ilijipatia umaarufu mkubwa baada ya kutengeneza simu zilizokuwa na ulinzi mzuri pengine kuliko simu nyingine zilizoko sokoni kwasasa. Hata hivyo kampuni hiyo ya Blackberry kwa sasa tayari inayo simu yake ya DTEK 50 ambayo inasemekana ni simu bora yenye ulinzi imara na pia ndio simu ya kwanza ambayo haijatengenezwa na kampuni hiyo ya Blackberry.

Ili kujua nini kitafuata juu ya kampuni hiyo ya Blackberry endelea kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube  ili kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Jiandae na Simu Mpya ya Samsung Galaxy M31
Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.