Pigo lingine tena limetokea kwa wapenzi wa tovuti za torrent baada ya tovuti ya torrentz.eu kufungwa, kiongozi wa tovuti hiyo ya torrentz hakusema lolote kuhusiana na hilo.
Hata hivyo wataalamu wa mambo wanasema hii ni kutokana na vita iliyo anzishwa hivi karibuni juu ya kudhibiti haki miliki za wasanii wa marekani akisema mmoja wa wapenzi wa tovuti hiyo marekani alisema kuwa tovuti hiyo imekua haiweki file au movie yoyote kwenye tovuti yake bali imekua ikiwawezesha watumiaji wa tovuti za torrent kupata link za kupakua sinema hizo hivyo sio haki kwa tovuti hii kufungiwa kama ndio hilo lililofanyika.
Tovuti hiyo kwa sasa inaonyesha ujumbe ambao unasema kuwa tovuti hiyo imeondolewa moja kwa moja, hili ni pigo tena kwa wapenda filamu baada ya kufungiwa kwa tovuti ya kickass torrent mwishoni mwa mwezi uliopita.
Kwa kupata habari zaidi unaweza kuungana nasi kupitia barua pepe (email) na tutakujulisha pindi tu habari mpya itakapo ingia kwenye tovuti yetu ya Tanzania tech, pia unaweza kutufuata kwenye mitandao ya kijamii ya facebook, Instagram, Twitter na Youtube Channel ili kupata video za habari na mafunzo ya teknolojia mbalimbali.