Video za Tetesi Zinazo Onyesha Simu Mpya ya iPhone 7

Video mpya inayo onyesha toleo la kwanza la simu ya iPhone 7
Iphone 7 Iphone 7

Kampuni ya Apple inc siku sio nyingi itatoa toleo lake jingine la simu yake mpya ya iPhone 7, simu hiyo inayotegemewa kutoka mwezi September tarehe 7 siku ya jumatano ikiwa zimebaki siku chache kwa simu hiyo kutoka baadhi ya tetesi zinasema simu hiyo ya iPhone 7 inategemewa kuwa na maboresho mengi pamoja na sifa nyingi mpya, hata hivyo blog nyingi za teknolojia nchini marekani zimeonekana kuiponda simu hiyo kutokana na kuondolewa kwa baadhi ya vitu kwenye simu hizo za iPhone 7.

Hata hivyo watu mbalimbali wameonekana kutoa tetesi mbalimbali kuhusu simu hiyo mpya inayotegemewa kutoka mwishoni mwa wiki inayokuja, hii ikiwemo video mbili kutoka kwenye mtandao wa youtube zimeonekana kuonyesha mfano wa matoleo hayo, video hizo zilizokua zikionyesha muonekano wa simu hizo zimeonekana kwa mara ya kwanza kwenye mitandao ya habari za teknolojia ya SlashGear pamoja na  Blog ya habari za teknolojia ya nchini japani ya Mac Otakara.

Ifuatayo ni video kutoka kwenye mtandao wa Slash Gear ikiwa inaonyesha muonekano huo wa kwanza (prototype) wa simu hizo za iPhone 7 na 7 plus.

Advertisement

Video nyingine inaonyesha simu hiyo ya iphone 7 ikiwa ina sifa mbalimbali kama vile kuto kuingia maji na sifa nyingine ambazo hazikwepo kwenye video ya kwanza hapo juu. Pia video hiyo ilikua ikionyesha mlinganisho wa iPhone 7 na iPhone 6.

Kama unataka kuonelea kujua kuhusu tetesi za simu hizi mpya pamoja na kuangalia live uzinduzi wa simu hiyo siku ya tarehe 7 mwezi September enelea kufuatilia blog yako mpya ya habari za teknolojia tanzania tech pia unaweza kupata habari za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa kupakua App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use