Samsung Galaxy Note 7 Yaja na Kioo Bora Pamoja na Iris Scanner

Simu mpya ya samsung galaxy note 7 yaja na teknolojia nyingi mpya pamoja na ulizi zaidi
Samsung Note 7 Samsung Note 7

Simu mpya ya Samsung Galaxy Note 7 ilizinduliwa jana huko nchini New York kama ulikosa kuangalia uzinduzi huo bofya hapa kuangalia tukio zima lilivyotokea hapo jana, uzinduzi wa samsung note 7 hapo jana ulipokelewa kwa namna ya tofauti sana na watu mbalimbali duniani kwani simu hiyo ambayo inaongezeka kwenye familia ya matoleo ya simu za samsung ya mwaka huu 2016 imekuja na teknolojia nyingi mpya pamoja na kuboreshwa zaidi.

Advertisement

Simu hiyo ambayo inasemkana kuwa na sifa sawa na za Samsung Galaxy S 7 imezinduliwa ikiwa na teknolojia mpya ya ulizi ijulikanayo kama Iris Scanner kwa wale msiojua iris scanner ni teknolojia ambayo inaongeza ulinzi kwa kunakili uso pamoja na macho yako maana yake ni kwamba endapo unataka kutumia simu yako ya samsung galaxy note 7 huna haja ya kutumia Pattern lock, Finger Print au Hata Password zozote za kawaida utakachofanya ni kusogelea kioo cha simu yako hiyo na simu yako itafunguka moja kwa moja.

Pia samsung Galaxy Note 7 imekuja na kioo ambacho ni bora zaidi cha kujikunja ambacho kinaonyesha picha angavu kikiwa kinasaidiwa na teknolojia ya Super AMOLED, simu hiyo itakuwa sokoni kuanzia tarehe 19 August na itapatikana kwa rangi za black, silver, na blue ambayo Samsung wanaita “Blue Coral, rangi ya Gold itapatikana kwa simu zitakazo uzwa nje ya marekani.

Kwa kupata habari zaidi unaweza kuungana nasi kupitia barua pepe (email) na tutakujulisha pindi tu habari mpya itakapo ingia kwenye tovuti yetu ya Tanzania tech, pia unaweza kutufuata kwenye mitandao ya kijamii ya  facebook, Instagram, Twitter na Youtube Channel ili kupata video za habari na mafunzo ya teknolojia mbalimbali.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use