Panasonic na Sony Zaungana Kutengeneze TV za 8K

Kampuni za Sony na Panasonic zimepanga kutengeneza TV za 8k ifikapo mwaka 2020
Teknolojia 8K Teknolojia 8K

Baada ya kufungwa kwa sherehe za Olympic huko brazil kampuni za sony pamoja na panasonic zimetangaza uhusiano rasmi ambapo uhusiano huo utakua wa kutengeneza TV zenye uwezo wa kuonyesha picha angavu za 8K, uhusiano huu utashirikisha kituo cha televisheni cha nchini japani cha NHK kituo ambacho kimeshafanya majaribio kadhaa ya kuonyesha michezo mbalimbali kwa kutumia teknolojia hiyo mpya ya 8K.

Hata hivyo kampuni hizo zimepanga kuonyesha matangazo ya michezo ya Olympic yatakayofanyika tena mwaka 2020 huko nchini tokyo kwa kutumia teknolojia hiyo mpya ya 8K ambayo kwa sasa ni adimu sana duniani. Inasemekana kuwa kuna aina moja tu ya TV yenye uwezo wa 8K ambayo imetengenezwa na kampuni ya Sharp ya nchini japan, TV hiyo inasemekana kuwa na 85-inch na ina dhamani ya dollar za kimarekani $130,000 sawa na Euro £100,000 sawa na shilingi za kitanzania TZS 286671959.07 hii ni kulingana na kiwango cha kubadilisha pesa cha tarehe 31-08-2016.

Kama unataka kuapata habari za TV hiyo pindi itakapotoka enelea kufuatilia blog yako mpya ya habari za teknolojia tanzania tech pia unaweza kupata habari za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa kupakua App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa video.

Advertisement

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use