Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Simu Tano 5 Bora za Kununua Mwaka 2016

Je Unatafuta Simu Bora ya Kununua Soma Hii Upate Kujua Simu Tano Bora za Mwaka 2016
simu bora simu bora

Simu ipi ni bora kununua mwaka 2016..? Tumeulizwa swali hili mara nyingi sana na watu mbalimbali ndio mana leo nimeamua kupitia kwenye hili ili kuweza kusaidia kujua ni simu ipi hasa ya kununua mwaka huu yani 2016, lakini kumbuka kuwa kwenye article hii hatutaenda kuchambua simu bora za kununua kwa upande wa model bali tutaenda kuchambua simu bora kwenye upande wa kampuni, hii inatokana na ubora wa simu zinazo tengenezwa na kampuni husika na pia hii inatokana na maoni machache ya watu kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania Moja kwa moja basi twende tuka hesabu simu hizi bora tani (5) za kununua mwaka 2016.

iPhone

Advertisement

iPhone

Nikisema iPhone ni moja kati ya simu ambazo mimi mwenyewe binafsi ningekushauri kununua nadhani watu wengi sana wangekubaliana na mimi kwa sababu, iPhone ni moja kati ya simu za kisasa zenye muonekano mzuri sana kama uko kwenye reli ya kutafuta simu zenye muonekano mzuri na pia tukizungumzia swala la quality iPhone ni moja kati ya simu zenye muonekano wa kisasa kabisa.

Kizuri kuhusu iPhone

  • iPhone ni simu yenye ubora wa kisasa kabisa kuanzia kamera, kioo na hata muonekano wake pia iPhone ni simu ambayo inakufanya uwe tofauti kidogo ukitegemea ni simu ambayo inauzwa kwa bei ya juu kiasi hasa kwa hapa tanzania, vilevile tunakubaliana kuwa ubora wa simu ni battery iPhone ni moja kati ya simu ambazo zimeonakana kufanikiwa kukaa na chaji kulio simu zingine zote.

Kibaya kuhusu iPhone

  • Kibaya kuhusu simu za iPhone ni bei simu hizi zimekuwa zikiuzwa kwa bei ya juu sana hii inafanya kwa wale watu wanaotafuta simu ambazo ni bora lakini wenye pesa ndogo kukosa wanachotaka pia vifaa vya simu hii ni shida kuvipata ni lazima kufika kwenye duka la iStore lililo karibu na wewe ili kupata kifaa kilicho bora na orignal.

 

Samsung

Samsung

Samsung ni moja kati ya simu ambazo zinatumiwa na watu wengi sana hasa kwa hapa tanzania kama unatafuta simu yenye kufanya kazi zaidi ya simu hakika samsung ni simu yako, pia zaidi ni kwamba vifaa vya simu hizi pamoja na teknolojia ya simu hizi ndio kitu kingine kinachofanya simu hii indelee kuwa bora na iwe namba mbili (2) kwenye list hii.

Kizuri kuhusu Samsung

  • Kama unatafuta simu ambayo inaweza kufanya kazi zaidi ya simu samsung ni simu yako, pia simu hii ni moja kati ya simu zinazo tumia teknolojia ya hali ya juu sana hasa kwenye upande wa programu edeshi yani (Operating System) vilevile simu hii ni moja kati ya simu zenye matoleo mengi sana hii ikiwa inamaanisha kuwa simu hii ipo kwa kila mtu kwa upande wa bei.

Kibaya kuhusu iPhone

  • Kama nilivyosema awali ubora wa simu sio tu kioo, muundo na muonekano la! simu ni battery na samsung imeonekana kuwa haikai na chaji sana tena hasa pale unapo tumia simu yako sana, unaweza kuweka simu yako kwenye chaji karibia mara mbili (2) kwa siku inategemea na matumizi yako.

 

Sony

Sony

Sony ni moja kati ya simu ambazo kwa sasa ni moja kati ya simu bora sana hasa kwa upande wa kamera, pamoja na muundo wake kwa ujumla, hata hivyo kwa muda sasa sony imekuwa ni simu ambayo ni bora saha kwenye multimedia simu hizi huwa na kamera yenye quality ya juu kabisa hivyo kama unatafuta simu yenye kufanya vizuri kwenye upande wa multimedia sony ni simu yako.

Kizuri kuhusu Sony

  • Aina ya muziki, sauti na picha inayotolewa na simu ya sony ni moja kati ya baadhi ya vitu vichache vinavyofanya simu hii kuendelea kuwa bora zaidi

Kibaya kuhusu Sony

  • Sony pia ni moja kati ya simu ambazo hazikai na chaji simu hizi nyingi zinauwezo wa kukaa na chaji kuanzia saa 13 hadi 15 programu za simu hii zimeonekana kuwa ndio chanzo cha simu hizi kutokukaa na chaji.

 

Huawei

Huawei

Huawei ni simu za kisasa zenye kutumia teknolojia ya kisasa kabisa simu hizi zinauwezo mzuri katika na nimoja kati ya simu ambazo zinapendwa na watu wengi sana hasa hapa tanzania, simu hizi zimeonekana kuweza kudumu kwa uda mrefu sana hivyo kama unatafuta simu yenye kudumu kwa muda mrefu huawei ni simu yako.

Kizuri kuhusu Huawei

  • Kama unatafuta simu ya bei rahisi na yenye kudumu hakika huawei ni simu yako kwani simu hizi zimeonekana kuweza kumudu hali sana unaweza uka dumu na simu hii kwa muda wa miaka 4 mpaka 5 inategemea na matumizi pamoja na utunzaji wako.

Kibaya kuhusu Huawei

  • Simu nyingi za huawei zinakuwa na matatizo madogo madogo kama vile programu kujifunga, kustak mziki kujizima na matatizo mengine, mara nyingine simu hizi zinaweza kustak kabisa kwa muda kuanzia masaa 24 mpaka 48.

 

HTC

HTC

HTC ni moja kati ya simu ambazo zina uwezo mkubwa sana pia simu hii na muundo mzuri sana na pia simu hii ni nyepesi kiasi kwamba inaweza kuwa ni rahisi kuibabe mahali popote pale pia simu hii inatumia teknolojia ya hali ya juu sana ili kufikisha sauti nzuri ambayo haifananishwi na simu nyingine yoyote hili.

Kizuri kuhusu HTC

  • Kizuri kuhusu simu hizi ni kwamba simu hizi zinatumia teknolojia ya Bit ambayo inawezesha simu hii kutoa sauti ya bora na nzuri sana.

Kibaya kuhusu HTC

  • Kibaya kuhusu simu ya htc ni kwamba simu hii inatumia vioo ambavyo ni laini sana ikitokea umeangusha simu yako anza kufikiria kununua kioo hta kama simu haijaanguka sehemu kubwa.

Ni matumaini yangu utakuwa umepata idea ya simu gani unaweza kununua kwa kuzingati kile unacho hitaji ila kumbuka simu yoyote sio simu mpaka iweze kukidhi matakwa yako sio wewe uhudumie simu kila wakati bali simu ikuhudumie wewe.

Kama umeipenda hii usisite kulike page yetu ya Facebook pamoja na Twitter ili kupata habari mpya pindi zinapotoka, pia kwa kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo unaweza ku subscribe kwenye Youtube Channel yetu hapa Tanzania tech blog. Pia usisahau kubofya hako ka-LOVE hapo chini ili ku-show love..!!

26 comments
    1. Asante kwa kutembelea blog yetu kuna model nying mbalimbali hivyo ni ngumu kuweza kutaja zote, Ila hizo ni baadhi tu ya brand ambazo zinaonekana kupendwa sana kwa sasa.

  1. Naitwa George Kihwelo Hakika jamaa mpo vizuri na mnaijua vizuri kazi yenu ninafaidika sana na ujuzi wenu mengi nimejua kuhusu simu na komputa endeleeni hivyo hivyo He simu ya phantom 6plus ina ubora gani?

    1. Karibu sana unaweza kujiunga na forum yetu ili kupata suluhisho la mambo yote ya teknolojia pale utakapo kwama.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use