in

Hizi Ndio Programu (Apps) 8 za Android za Muhimu Kuanazo

Jaribu Programu Hizi Ili Kurahisisha Maisha Yako Kila Siku

Programu

Kama tunavyotambua ya kuwa siku hizi teknolojia imekua ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku, temekua tuki itumikia teknolojia na teknolojia imekua ikitutumikia yote hayo ni ili kurahisha maisha yetu kila siku, hapo ndipo panapo kuja matumizi ya simu za mkononi maarufu kama smartphone simu hizi zimekua ni msaada kwetu kwa namna moja ama nyingine zimetusaidia kuanzia kurahisisha maisha mpaka kujikwamua katika janga zima la kukosa kazi pamoja na ajira, tume shuhudia watu wengi waki jiajiri kutokana tu na uwepo wa smartphone hivyo basi umuhimu wa smartphone umekua ni mkubwa sana katika jamii yetu hii ya sayansi na teknolojia.

Hata hivyo uwepo wa smartphone pekee bila uwepo wa programu (Apps) mbalimbali kwenye simu hiyo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu hivyo basi leo tanzania tech tunakuletea programu hizi Nane 8 bora ambazo zimekua ni msaada mkubwa kwa watanzania wote kwa ujumla, kumbuka tu programu hizi nyingi hazi kuwepo kipindi cha nyuma hivyo kawambie na wengine ili waje wazipakue ili wote kwa pamoja turahisishe maisha.

Tanesco Huduma

Tanesco Huduma
Price: To be announced

Tanesco Huduma inawawezesha wateja kuripoti matatizo mbalimbali wanayopata wateja wa kinondoni north(Tegeta,Mikocheni,Mbezi beach) pamoja na kuripoti matatizo yanayo husisha huduma ya umeme ikiwamo kukatika kwa umeme,kudondoka kwa nguzo n.k. Vilevile wateja wataweza kupata ratiba za ukatikaji umeme kwenye Maeneo yao,kushugulikiwa matatizo yao kupitia huduma hii,bei za huduma mbali mbali za Tanesco na Tarifa zinazohusu shirika la umeme Tanzania.

Makini App

MakiniApp
Price: Free

Makini App ni programu itakayo kusaidia kujua speed ya gari ulilopanda ili kuweza kusaidia kupunguza ajali za barabarani, app hii inauwezo mzuri wa kutuma taarifa kwa askari wa usalama barabarani ili kuweza kuripoti dereva anaendesha gari kwa mwendo kasi pia kwa kutumia app hii unaweza kujua na kuona mahali gari linapoenda ili kujua umbali wa safari yako pale unaposafiri.

Hizi Hapa Apps ambazo ni Mbadala wa Soko la Play Store

Veta Somo

Vsomo
Price: Free

Kama tulivyo andika kwenye makala iliyopita kuhusu veta somo ni programu itakayo kusaidia kujifunza mafunzo ya ufundi stadi ili kuweza kujipatia ujuzi pamoja na cheti kutoka chuo cha mafunzo ya ufundi stadi tanzania yani VETA  hii itakusaidia kujiajiri au kujipatia ajira kuyokana na cheti hicho kutoka VETA.

Rifaro

Rifaro
Price: Free

Kwa kutumia app hii ya rifaro unaweza kuanzisha biashara kwa kiasi kidogo sana cha pesa programu hii ni sehemu ya mtandao wa kampuni ya Rifaro Africa ambayo ndio inaendesha biashara hii ya kuwawezesha wajasiriamali kuanza biashara unaweza kutembelea tovuti yao ya Rifaroafrica.com ili kujua namna ya kujiunga na mtandao huo.

Time Ticket

TiME Tickets
Price: Free

Programu Hii inarahisisha katika ununuaji wa tiketi za matamasha mbalimbali yanayo fanya hapa dar es salaam na tanzania kwa ujumla app hii ni nzuri na imeonyesha kusaidia watu wengi sana hii ni kwa mojibu wa komenti zinazopatikana kwenye ukurasa wa programu hii kwenye Google Play Store.

Smart Malipo

SmartMalipo
Price: Free

Programu hii inayotoka kwa wale mabingwa wa malipo MaxMalipo ni zaidi ya App kwani kwa kuwa na programu hii utaweza kuanzisha biashara yako ikiwa ni pamoja na kujipatia kamisheni kwa kila muamala utakaofanya kupitia programu hii, ina maana unaweza ukawa unanunua umeme wako na kufanya malipo na bado ukawa unapata kamisheni za miamala yote hiyo unayo ifanya. Zaidi ni kwamba huduma zote za malipo zinapatikana pamoja na uwakala wa vodacom. ni rahisi kutumia na huduma kwa wateja inapatikana muda wote.

WhatsApp Yaleta Uwezo wa QR Code Kwenye WhatsApp Business

Start MySafari

StartMySafari
Price: To be announced

Hii ni programu ambayo wengi wetu tunaijua sana lakini watu wengi wanasahau umuhimu wake mpaka kipindi cha kusafiri programu hii inauwezo wa kusaidia kukata tiketi ukiwa nyumba au offisini moja kwa moja kwa kutumia simu yako ya mkononi smartphone programu hii imeonekana kurahisisha maisha ya watanzania wengi na ni moja kati ya programu ambazo ni muhimu sana kuwa nazo kwenye smartphone yako.

Ajira Job Matching

Ajira - Job Matching

Kama unatafuta kazi na bado hujapata Ajira job matching ni programu ya kuwa nayo kwenye smartphone yako kwanu utapata taarifa za kazi mpya kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya kazi hapa tanzania hivyo ningependa kukushauri kuwa na programu hii kwenye simu yako kwani inasaidia sana.

Na hizo ni baadhi tu ya programu za muhimu kua nazo kwenye simu yako zipo programu nyingi sana ambazo ni muhimu sana kwepo kwenye smartphone yako tujulishe ipi ni muhimu kwako kwenye komenti ili tuiongeze kwenye list hii.

Kwa kupata habari zaidi unaweza kuungana nasi kupitia barua pepe (email) na tutakujulisha pindi tu habari mpya itakapo ingia kwenye tovuti yetu ya Tanzania tech, pia unaweza kutufuata kwenye mitandao ya kijamii kwenye facebook, Instagram, Twitter na Youtube Channel ili kupata video za habari na mafunzo ya teknolojia mbalimbali.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maoni 2

Toa Maoni Hapa
  1. Kuna App nyingine Inaitwa Pamoja app. Nayo pia imetengenezwa Tanzania. Ni social network app Na ni nzuri sana tofauti na nyingne nilizowahi kutumia. Inapatikana Playstore

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.