in

Nokia P1 Simu Mpya Kutoka Nokia Yenye Kutumia Android

Simu Hii Mpya Kutoka Nokia Inategemewa Kuingia Sokoni Mwaka Huu 2016

Nokia P1

Tokea mwezi may ambapo kampuni ya Nokia ilitangaza rasmi kurudi katika biashara ya utengenezaji wa smartphone tetesi mbalimbali zimekua ziki zaga mitandaoni. Hadi kufikia mwezi July picha mbalimbali zimekua ziki zagaa katika mitandao mbalimbali ambapo picha hizo zimeonekana kuonyesha simu ambayo ina logo ya Nokia ambayo ndio inadhaniwa kuwa ndio simu mpya ya kutoka kampuni hiyo kongwe ya Nokia.

Picha hizo ambazo zimeleta zogo sana mtandaoni baadae zilionekana kuwa ni za simu kutoka katika kampuni ya Sharp ijulikanayo kama Sharp Aquos P1, hata hivyo tetesi zinasema kuwa simu hiyo kutoka kampuni ya sharp ndio itakayo badilishwa na kuwa simu mpya ya Nokia P1 hata hivyo kampuni ya sharp haijazungumzia lolote kuhusu hilo.

Habari za tetesi kutoka blog mbalimbali za teknolojia zinaendelea kusema kuwa simu hiyo mpya ya Nokia P1 inategemewa kuja na 5.3-inch Full-HD display, Snapdragon 820 processor pamoja na 3GB RAM pamoja na 32GB expandable storage pia simu hiyo inategemewa kuwa na kamera ya 22.6MP primary camera pamoja na battery ya 3,000mAh, pia simu hiyo inategemewa kuwa na teknolojia ya fast charging na IP58 dust pamoja na waterproof.

ZTE Axon 20 5G : Simu ya Kwanza Yenye Kamera Chini ya Kioo

Hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa tetesi kama hizi kuzagaa mtandaoni hapo mwanzoni mwa mwaka huu tetesi zilisambaa kuhusu simu mpya ya Nokia C1 ambayo ilikuwa itengenezwe kwenye mifumo yote miwili ya Android pamoja na Windows, hata hivyo tetesi hizi zilibaki kuwa tetesi na hakukua na simu yoyote iliyotolewa na kampuni hiyo maarufu. Hata hivyo vyanzo mbalimbali vya habari vinadhibitisha kuwa Nokia imeshaanza kutengeneza Simu yake yenye kutumia Android, hivyo hivi karibuni watu wategemee kuona simu kutoka kampuni hiyo kongwe kutoka finland.

Kwa kupata habari zaidi unaweza kuungana nasi kupitia barua pepe (email) na tutakujulisha pindi tu habari mpya itakapo ingia kwenye tovuti yetu ya Tanzania tech, pia unaweza kutufuata kwenye mitandao ya kijamii kwenye facebook, Instagram, Twitter na Youtube Channel ili kupata video za habari na mafunzo ya teknolojia mbalimbali.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.