Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

“Mesuit” Kava Lenye Uwezo wa Kubadili iPhone Kuwa Android

Kwa kupachika Kava hili utakuwa na uwezo wa kutumia Android kwenye simu yako ya iPhone
Cover la Mesuit Cover la Mesuit

Hivi karibuni huko nchini china uwezo wa kuwa na Android na iOS kwenye simu moja umedhiirika wazi kwa kutengenezwa kava la Mesuit, kava hili linauwezo wa kubadili simu yako ya iPhone na kuwa Android kwa wakati mmoja.

Advertisement

Hii sio mara ya kwanza kwa baadhi ya makampuni kujaribu kuunganisha Mifumo hiyo ya uendeshaji ya smartphone, mwezi uliopita mbunifu kutoka katika kampuni ya Tendigi Nick Lee alifanya ubunifu unao fanana na huu kwa kutengeneza kava lenye sakiti ambayo ilikua likiwezesha mfumo wa Android Marshmallow kufanya kazi kwenye simu za iPhone. Hata hivyo mbunifu huyo akuwa na lengo la kuingiza bidhaa hiyo sokoni.

Baada ya Mr Lee sasa kampuni ya China ya Haimawan  imefanikiwa kutengeneza kava la Mesuit ambalokwa sasa lipo sokoni kwenye tovuti ya Jijia’s ya nchini china, Hata hivyo akizungumzia jinsi linavyofanya mmoja kati ya wataalamu wa kampuni hiyo walisema kuwa kava hilo linauwezo wa kutumia kuendesha android kwenye simu za iPhone 6 na kuendelea pia mfumo huo wa uendeshaji unauwezo wa kutumiaka kama programu (App) ambayo ujiweka mara tu unapopachika kava hilo.

Kava hilo pia linakuja na battery ya ziada ya 1,700mAh kwa iPhone 6 pamoja na 6 Plus battery ya 2,500mAh pia kava hilo lina kuja na memory ya ziada ya GB 16 likiwa na sehemu ya kupachika line nyingine za simu. Kava hilo kwa sasa linauzwa kwa nchini china kupitia tovuti ya Jijia’s kwa kiasi cha ¥999.00 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania TZS 329550.00 kwaajili ya  iPhone 6 pamoja na 6S, pia ¥1099.00 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania TZS 22755.80 kwa iPhone 6 Plus na 6S Plus. Hata hivyo kampuniya Hamawan bado haijasema lolote kuhusu kuuza kava ilo nje ya mipaka ya china.

Kwa kupata habari zaidi unaweza kuungana nasi kupitia barua pepe (email) na tutakujulisha pindi tu habari mpya itakapo ingia kwenye tovuti yetu ya Tanzania tech, pia unaweza kutufuata kwenye mitandao ya kijamii ya  facebook, Instagram, Twitter na Youtube Channel ili kupata video za habari na mafunzo ya teknolojia mbalimbali.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use