OLED TV ni televisheni za kisasa ambazo hutumia teknolojia ya kisasa iitwayo OLED au (Organic Light Emitting Diodes), Mara nyingi televisheni zinazo tumia teknolojia hii huwa ni nyembamba pia huonyesha picha angavu kwa kifupi ni kwamba televisheni hizi huwa zenye ubora sana hasa ikija katika swala la picha pamoja na muonekano.
OLEDs hutengenezwa kwa kuwekewa plastic nyembamba za carbon ambazo ni organic (carbon based) plastic hizi huwekwa kati ya conductors ambapo pale umeme unapopita kati ya conductors hizo mwanga angavu hutengenezwa na hii kuleta mng’ao wa picha, tofauti na televisheni za LCD OLED TV haiitaji mwanga wa ziada ili kungarisha picha yake kwani kila pixel ya screen ya OLED TV inatengeneza mwanga wake yenyewe yaani (small light-emitting diode).
Hata hivyo kuna faida mbalimbali za kutumia televisheni zenye teknolojia hii ya OLED, zifuatazo ni kati ya faida hizo chache za kutumia OLED TV
- Ubora wa picha rangi pamoja na mwanga wa kioo.
- Nyembamba na Nyepesi, OLED TV nyingi huwa kati ya 4 mm na 0.3 mm (hizi zikiwa ni OLED panel ambazo ni prototypes yani ziko kwenye majaribio).
- Kuna uwezekano mkubwa wa kuangalia OLED TV kwa upande hadi kufikia nyuzi 180 degrees.
- OLED TV nyingi hazitumii kiwango kikubwa cha umeme hivyo kusaidia kupunguza kiwango cha madhara yatokanayo na madini yapatikanayo kwenye screen hizo, kwa mfano OLED TV zina madini kidogo ya Iridium ambayo hayana madhara yoyote kwa binadamu.
- Pia OLED TV nyingi huwa zimetengezwa kwa ubora wa hali ya juu kuanzia kioo mpaka muundo wake.
Hata hivyo kampuni ya LG ndio moja kati ya kampuni chache zinazojihusisha na utengenezaji wa televisheni hizo zinazotumia teknolojia hiyo ya OLED.
Kwa kupata habari zaidi unaweza kuungana nasi kupitia barua pepe (email) na tutakujulisha pindi tu habari mpya itakapo ingia kwenye tovuti yetu ya Tanzania tech, pia unaweza kutufuata kwenye mitandao ya kijamii kwenye facebook, Instagram, Twitter na Youtube Channel ili kupata video za habari na mafunzo ya teknolojia mbalimbali.