Mkutano Mkubwa wa Apple WWDC Kufanyika June 13

Apple WWDC Apple WWDC

Kama inavyofanyika kila mwaka watengenezaji (developer) kote duniani wanajumuika kwenye mkutano mkubwa wa Apple ambao unakua ukizungumzia mambo mbalimbali yanayohusiana na bidhaa za apple, mkutano wa mwaka huu utafanyika June 13 huko San Francisco nchini marekani.

Kinachotegemewa kwenye mkutano huo ni uzinduzi wa simu mpya ya iPhone 7 pamoja na programu mpya ya Mac OS ambapo watu wategemee kubadilika kwa jina kutoka OS X kuwa Mac OS , pia uzinduzi wa progamu mbalimbali za simu hiyo unategemewa sana ukizingatia kuna baadhi ya programu zilizo zinduliwa kwenye uzinduzi wa iPhone SE lakini bado hazijawafikia watumiaji, pia tetesi zinasema kuwa programu ya SIRI itaongezewa ufanisi wa kazi ili kuweza kupokea simu, kujibu meseji na mambo mengine mbali na zaidi ni kuwa inasemekana kuwa watengenezaji watapewa uwezo wa kutengeneza programu mbalimbali ambazo zitakua zikifanya kazi kwenye sambamba na programu hiyo ya siri, hii ni kwa kutumia uanzishwaji mpya wa SIRI API.

Tutakua tukionyesha Live mkutano wote utakapokua ukifanyika hivyo pitia blog hii mara kwa mara kupata habari kuhusu mkutano huo mkubwa wa watengenezaji wa Apple WWDC.

Advertisement

Kama umeipenda hii usisite kulike page yetu ya Facebook pamoja na Twitter ili kupata habari mpya pindi zinapotoka,pia kwa kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo unaweza ku subscribe kwenye Youtube Channel yetu hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use