Lenovo Yaonyesha Simu zake Zenye Kioo cha Kujikunja

Video Ikionyesha Mtangazaji Maarufu Meghan McCarthy Akionyesha Simu Mpya za Lenovo
Simu za Lenovo Simu za Lenovo

Tumesha sikia kwa muda mrefu kuwa simu zenye kioo cha kujikunja au Flexible Display zinategemea kuingia sokoni hivi karibuni, lakini kampuni ya Lenovo leo imeamua kuondoa subiri hiyo kampuni hiyo imezindua na kuonyesha simu na tablet zenye uwezo wa kioo cha kujikunja au Flexible Display.

Kampuni hiyo maarufu ilifanya uzinduzi huo kwenye mkutano ujulikanao kama World keynote uliofanyika leo huko marekani kampuni hiyo ya lenovo ilimuomba mmoja kati ya washiriki wa mkutano huo kuonyesha bidhaa hizo mpya za lenovo ambapo mshiriki huyo alitoa simu na kuifunga kwenye mkono wake wa kulia kama saa, pia mshiriki huyo alitoa tablet na kuikunja ili-kuwa kama simu ya kawaida. Hata hivyo lenovo wanasema kuwa simu hizo zitawafikia watu hivi karibuni na kwa sasa zipo zinaonyeshwa kwenye maonyesho ya mkutano huo wa World convention huko marekani.

Advertisement

Unaweza cheki video ya tukio hilo hapo juu. Kama umeipenda hii usisite kulike page yetu ya Facebook pamoja na Twitter ili kupata habari mpya pindi zinapotoka, pia kwa kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo unaweza ku subscribe kwenye Youtube Channel yetu hapa Tanzania tech blog.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use