Prophix Mswaki Unaoweza kukuonyesha Ndani ya Mdomo Wako

Prophix Mswaki Unaoweza kukuonyesha Ndani ya Mdomo Wako Prophix Mswaki Unaoweza kukuonyesha Ndani ya Mdomo Wako

Madaktari wengi nchini marekani wanashauri ya kuwa ni vyema kutumia mswaki wa umeme kuliko kutumia mswaki wa kawaida au kwa jina lingine mswaki wa mkono, hii ni kwasababu kuna uwezekano mkubwa wa kushindwa kusafisha meno yako yote kwa usahihi kutokana na hayo mswaki ambao unatarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni wa Prophix ni mswaki uliolenga kukusaidia kuimarisha afya ya kinywa na meno yako kwa urahisi kabisa.

Mswaki huu uliotengenezwa na kampuni ya Onvi ya nchini marekani unauwezo wa kukusaidia kuona ndani ya kinywa chako wakati ukiswaki, ili kuwezesha hilo mswaki huo umetengenezwa na kamera maalumu ambayo iko mbele ya mswaki huo ambayo ndio inayokusaidia kurekodi video ya ndani ya kinywa chako na kuonyesha moja kwa moja kwenye simu yako. Hata hivyo wataalamu hao wanasema ili kusudi uweze kutumia mswaki huo inakubidi kupakua programu maalumu ambayo ndio itakusadia kuweza kuonyesha video hizo kutoka katika kinywa chako pitia mswaki huo, zaidi ni kwamba unaweza kuchukua picha ya kawaida (picha ya mnato) ya meno yako kwaajili ya kumuonyesha daktari pale utakapo hisi kuna tatizo kwenye kinywa chako.

Advertisement

Mswaki huo utauzwa kuanzia dollar za kimarekani $400 au zaidi hata hivyo bado mswaki huo haujaingia sokoni rasmi ila unapatikana moja kwa moja kwenye website ya kampuni hiyo ya Onvi. Kwa info zaidi cheki video hapo juu

Kama umeipenda hii usisite kulike page yetu ya Facebook pamoja na Twitter ili kupata habari mpya pindi zinapotoka, pia kwa kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo unaweza ku subscribe kwenye Youtube Channel yetu hapa Tanzania tech blog.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use