Instagram Yapanga kuleta Akaunti za Kibiashara

Instagram Bussiness Instagram Bussiness

Mtandao maarufu wa instagram mwanzoni mwa mwaka huu ulitoa ripoti yakuwa unafanyia kazi toleo jipya la instagram ambalo litakua na akaunti za kibiashara, toleo hilo jipya litamwezesha mtumiaji wa instagram kuwa na profile ya biashara kama ilivyo katika facebook.

Akaunti hizo zitakuwa tofauti kabisa na zile za kawaida tunazo ziona kila siku kwani zitakuwa na sehemu maalumu ya kuchagua aina ya biashara pia sehemu ya kuweka mawasiliano pamoja na sehemu maalumu ya kujaza mahali biashara ilipo.

Mpaka sasa zipo baadhi ya akaunti ambazo tayari zimesha wekwa kama page za kibiashara kwaajili ya kufanyiwa majaribio, msemaji mkuu wa mtandao huo alisema kuwa watu wategemee kupata toleo hilo jipya ndani ya miezi michache inayokuja.

Advertisement

 

3 comments
  1. Hii blog imetulia sana unaweza uka cheki blog yangu na mimi inaitwa www.bongomusicsearch.com ni kwaajili ya muziki unaweza ukatafuta mziki wowote hapo

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use