Youtube Yaleta Aina Mpya ya Matangazo

Youtube Yaleta Aina Mpya ya Matangazo Youtube Yaleta Aina Mpya ya Matangazo

Kampuni ya Google kupitia mtandao wake wa kijamii wa YouTube imetangaza kupitia blog yake kuwa sasa kuna aina mpya ya matangazo ambayo yatakua yakitokea kama video fupi ya sekunde 6, habari hizo zilizo andikwa na meneja wa bidhaa hapo YouTube Mr Zach Lupei zinasema matangazo hayo ni sehemu ya mpango kazi wa kuboresha mtandao huo maarufu kwa kushare video wa YouTube.

Hata hivyo blog hiyo iliendelea kuandika kuwa watumiaji wa mtandao huo hawatakua na uwezo wa kusogeza (SKIP) matangazo hayo kwani yanatokea kwa muda mfupi sana hivyo kutakua hakuna haja ya kuyasogeza (SKIP) matangazo hayo iliandika sehemu ya habari kwenye blog hiyo. Hata hivyo hii ni habari njema kwa wale wanaoonyesha matangazo kwenye channel zao kwani hii inamaanisha kuongezeka kwa mapato kutokana na matagazo hayo mafupi maarufu kama “Bumper Ads“.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use