in

YouTube Imetangaza Kuanza Kuonyesha Video za Live za 360

Youtube imetangaza kuanza kutoa huduma ya kuonyesha video za nyuzi 360 lakini kumbuka video zitakazo weza kuonyeshwa kwa teknolojia hiyo ya nyuzi 360 ni zile za moja kwa moja ama kwa jina lingine  “Live Streaming” , Pia kampuni hiyo imetangaza kuzindua huduma nyingine ya sauti ijulikanayo kama “spatial audio” teknolojia hii ina saidia kuimarisha sauti hasa ya video au audio zinazo rekodiwa moja kwa moja au Live.

Hata hivyo tayari watu wameshaanza kuonyesha matamasha mbalimbali kwa kutumia teknolojia hiyo mpya ambayo hata ukiwa na smartphone yako ya galaxy S7 pamoja na Gear 360 tu unaweza kurekodi video hiyo ya nyuzi 360. Kumbuka ili kuweza kutengeneza video ya nyuzi 360 ni lazima uwe na kifaa chenye teknolojia hiyo ya 360 lakini katika upande wa kuangalia video hizo huna haja ya kuwa na kifaa cha ziada unaweza kutumia vifaa vya kawaida tu kama kompyuta ama Simu yako ya mkononi.

Tizama mfano wa video hiyo hapo juu kisha bofya vitufe vilivyoko juu upande wa kushoto kuagalia nyuzi 360.

Tovuti Bora za Kusaidia Kudownload Nyimbo za Dini kwa Urahisi
Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.