in

‘Smarttress’ Kitanda Kinachofanya Ugundue Kama Mkeo Anakusaliti

Je unataka kugundua kama mkeo anakusaliti..? sasa ni rahisi kampuni inayotengeneza vitanda vinavyotumia Wi-Fi ya Durmet sasa imetengeneza kitanda ambacho kinatumia sensa “Sensor” ambazo zinakupa uwezo wa kugundua kama kitanda chako kimelaliwa na mtu mwingine, kitanda hicho kinauwezo wa kutuma taarifa mbalimbali za siku nzima kuhusiana na kitanda chako moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi.

Kitanda hicho kilichotengenezwa na ultrasonic sensors zaidi ya 24 kitauzwa kwa dollar za kimarekani zaidi yaUSD  $1,750 hata hivyo kitanda hicho kimetengenezwa kwa spring ambapo katikati ya pring hizo ndipo kulipo na Sensor hizo zinazoweza kukupa taarifa za kitanda chako kama kimelaliwa na mtu mwingine.

Kazi kwenu kwa mnao hisi ukitoka kuna mtu anaingia, kitanda hichi kitakua bonge la msaada ila sijui pale sensor zinapo isha chaji na ndo siku hiyo njemba linakuja nyumbani kwako duh, kujua zaidi cheki video ya kitanda hivho hapo juu pia unaweza kupitia website ya watengenezaji wa kitanda hicha hapa Durmet .

Jinsi ya Kuona Namba za Simu za Mtu Unaechati Nae Facebook
Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maoni 1

Toa Maoni Hapa

    Toa Maoni Hapa

    Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.