in

‘Melomind’ Spika za Kichwa Zenye Uwezo wa Kufundisha Kupumzika

Kutana na ‘Melomind’ spika hizi za kichwa (Headphone) zina uwezo mkubwa wa kukufanya upumzike vizuri na kuondoa msongo wa mawazo, spika hizi zinafanya kazi zaidi ya kucheza muziki kwani zinakuja na kifaa maalumu (Sensor) kiitwacho (Electroencephalographic Sensors) kifaa hichi kinauwezo wa kusoma ubongo wako na kutoa muziki kwa namna ya aina yake ili kukusaidia kupumzika vizuri na kuondoa msongo wa mawazo.

Kifaa hichi kinacho tangazwa na website maarufu ya Kickstarter kinatumia miozi ya bluetooth kuunganisha na simu yako ya mkononi hata hivyo ili kupata taarifa za ubongo wako itakubidi kupakua programu maalumu ya Android au iOS ili kupata taarifa hizo moja kwa moja kutoka katika kifaa hicho kipya. Watu wengi duniani walio pata nafasi ya kujaribu kifaa hicho walionekana wakipunguza mawazo na kupumzika vizuri ndani ya dakika 5 tu.

Kifaa hicho kitapatikana kwa dola za kimarekani kati ya USD $280 au Pungufu, pia kampuni hiyo inasema kifaa hicho kitaanza kusafirishwa na kupatikana kote duniani kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Kampuni ya Nokia Yazindua Simu Mpya ya Bei Nafuu ya Nokia 2.2
Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.