in

Facebook Yafikisha Watumiaji Bilioni 1.65 kwa Mwezi

Kampuni kubwa ya facebook imezidi kuongoza na kukimbiza makampuni mengine ya teknolojia duniani, hivi karibuni kampuni hiyo imetoa ripoti ya kwanza ya nusu mwaka 2016 ambapo ripoti hiyo ilikua ikionyesha kuongezeka kwa mapato ya kampuni hiyo pamoja na kuongezeka kwa watumiaji wa mtandao wake mpaka  kufikia watumiaji Bilioni 1.65 kwa mwezi.

Kampuni hiyo iliandika kwenye ripoti yake hiyo kuwa mapato ya kampuni hiyo yameongezeka mpaka dollar za kimarekani bilioni $5.38, hata hivyo kampuni hiyo inapata makadirio ya dollar za kimarekani $0.77 kwa kila share inayofanyika kwenye mtandao wake wa facebook. Mapato hayo yameongezeka kwa kasi sana mojibu wa ripoti hiyo kutoka asilimia 2% mpaka asilimia 8%. Hata hivyo mapato ya facebook yameonekana yakiongezeka kwa asilimia 57 kila mwaka haya ni mabadiliko makubwa sana ya mapato, facebook inaendelea kuongeza gharama ya hisa zake kote duniani.

Tovuti Bora za Kusaidia Kudownload Nyimbo za Dini kwa Urahisi
Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maoni 1

Toa Maoni Hapa

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.