Apple Inaweza Kubadili Jina la Programu Yake ya OS X na Kuwa ‘MacOS’

Apple Inaweza Kubadili Jina la Programu Yake ya OS X na Kuwa 'MacOS' Apple Inaweza Kubadili Jina la Programu Yake ya OS X na Kuwa 'MacOS'

Hivi karibuni kuna habari mbalimbali kutoka kwenye blog tofauti za teknolojia zinazosema kuwa kampuni maarufu ya Apple imepanga kuachana na jina la programu yake ya kompyuta zake maarufu kama OS X, habari hizo zinaendelea kusema kuwa kampuni hiyo imepanga kutumia jina la “MacOS “au macOS ikiwa na herufi ndogo.

Pia inasemekana kuwa Jina hilo litazinduliwa rasmi kwenye mkutano maalumu wa WWDC (Apple Worldwide Developers Conference) ambao utafanyika mwezi june mwaka huu huko San Francisco. Hii sio mara ya kwanza kwa kampuni ya Apple kubadilisha majina ya programu zake hizo, hapo awali programu hizo zilikua zikiitwa “Mac OS X” na baadae kampuni hiyo iliachana na jina la kwanza la programu hiyo yani “Mac” na kutumia jna la “OS X”  ambalo mpaka saa ndilo linalotumika.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use