in

Namna ya Kufanya Ma-folder ya Computer yako Kufunguka Haraka

Tatizo la computer nyingi kufungua mafolder taratibu ni kubwa sana hata kwa watumiaji wa computer wenye computer zenye uwezo mzuri, lakini kuna njia rahisi sana ya kufanya mafolder yako katika computer yako kufunguka haraka.

Je ni kwanini mafolder yanafunguka taratibu kwenye computer yako na tena hasa mafolder yenye picha ama movies.?

Katika toleo la zamani la window yani window vista kulikua na sehemu ambapo unaweza kutenganisha kuwa mafolder yako yana hifadhi vitu vya aina gani, lakini sasa window inafanya kazi automatic yani kama folder lina picha window itagundua kwamba hili folder lina picha hivyo itaenda moja kwa moja kuseti folder lako katika fomati ya picha, mfumo huu unategemeana na kiasi cha ma-file ulioweka kwenye folder lako kama umeweka picha nyingi katika folder moja window itaweka folder lako katika mfumo wa picha hivyo hivyo pia kwenye video kama video ni nyingi itaweka format ya folder lako kuwa folder la video.

Pindi option hii inapofanya kazi huwa ni nzuri na ufanya kazi bila wasiwasi ila kama option hii haifanyi kazi ndipo utakapo anza kuona ma-folder yako yakisoma kwa taratibu kama inavyo onekana hapo kwenye picha.

Jinsi ya Kutumia USB Flash Kwenye Simu ya Android

ximg_56eb3462d8d65.png.pagespeed.gp+jp+jw+pj+js+rj+rp+rw+ri+cp+md.ic.BKDyH5R-31

Je unafanyaje ili kufanya Mafolder yako hayo kufunguka kwa haraka sana.? Kwa bahati nzuri namna ya kufanya mafolder yako yasome kwa haraka ni rahisi sana kama utakua unajua ni wapi pakuangalia.

Tafuta Folder lenye tatizo la kufunguka kwa taratibu kisha select folder lako kisha bonyeza kibonyezo cha kulia cha mouse yako kisa chagua Properties.

download

Ukiwa ndani ya properties Menu changua Customise.

ximg_56eb367c74d09.png.pagespeed.gp+jp+jw+pj+js+rj+rp+rw+ri+cp+md.ic.aA70wc7E4s

Kwenye Customise utakuta kuna option imeandikwa “Optimize this folder for:” kwenye option hiyo chini ya maandishi hayo bonyeza katika ya kibosi na utaona machaguzi haya “General items”, “documents”, “pictures”, “music”, na “videos” wewe chagua “General items”.

m

Kisha weka tika kwenye option iliyo andikwa “Also apply this template to all subfolders” sehemu hii iko chini kidogo ya menu tulio chagua awali.

m3

Kisha bonyeza “Apply” alafu bonyeza “OK” inayopatika chini kabisa mwisho, kisha bonyeza F5 ili kurudia kufungua folder lako.

m5

Baada ya hapo folder lako sasa litakua linafunguka kwa haraka kabisa bila tatizo lolote, njia hii ni rahisi kufuata na kama unaona umeshindwa kufuatilia njia hizi tafanyali angalia video hapo juu.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.