in

Facebook Messenger ni Zaidi ya Kuchati

Watu wengi hutumia Facebook Messenger kwa ajili ya kuchati na ndugu na jamaa lakini sio watu wote wanao jua kuwa Facebook Messenger inaweza kufanya kazi zaidi ya kuchati, Application hii ya facebook inazo application ndani yake ambazo zitafanya utumie app hiyo zaidi ya kuchati na kufurahia kuwasiliana na ndugu na jamaa kwa namna ya aina yake.

Mwaka jana facebook ilitangaza kuanzisha utengenezaji wa application ndani ya Facebook Messenger ambazo zina uwezo wa kutumika ndani ya application hiyo, zifuatazo ni game application tano bora zinazoweza kubadilisha jinsi unavyotumia application hiyo ya Facebook Messenger.

Pakua Facebook Messenger hapa kwa wale wenye iOS ili uweze kucheza game hizi zinazopatikana ndani ya Facebook Messenger.

[appstore id=454638411]

Chess

Mwezi uliopita watumiaji wa application ya facebook messenger waligundua application iitwayo Chess application game hii inaweza kuchezwa na watu wawili kama vile inavyokuwa katika chatting za application hiyo. Ili kuanza kucheza game hiyo na rafiki yoyote kwenye application ya FB Messenger andika “@fbchess play.” pia mtumiaji anaweza kuandika “@fbchess help” ili kupata msaada na maelekezo namna ya kucheza game hiyo kwenye Facebook Messenger.

Fahamu Njia Rahisi ya Kujua Mapato na Matumizi Yako

Kwenye game hilo P inasimama badala ya “Pawn”, R inasimama badala ya “Rook”, B badala ya “Bishop” na Q badala ya “Qeen”, K badala ya “King” na Kuendelea kwa watalamu wa chess hapa watakua wanajua nazungumzia nini.

Doodle Draw

Mchezaji wa game hii anaweza kuchora kitu pale mchezaji wapili anapojua ni nini alichochora hapo atajipatia Point pale anaposhindwa kujua ni kitu gani mchoraji hujupatia Point.

Basketball

Game hii imekuja hivi karibuni kwenye Facebook Messenger game hii inaanza pale mtumiaji anapo tuma emoji ya basketball kwenda kwa mtumiaji anaetaka kucheza nae game hii, Slide vidole kwenye screen yako utaona mpira wa basketball ukiruka kuingia kwenye nyavu. Pale unapokosa inatoke emoji ya mtu alioko na majonzi pale unapopatia inatokea emoji ya mtu alie na furaha hapo unakua umepata point.

Giphy

Game hii unaweza kumtumia mwenzako picha zinazo cheza yani GIF na mchezaji wa pili anaweza na yeye akakutumia hivyohivyo, ni game zuri na inaweza kukufanya usitoke kwenye simu yako kirahisi.

Kampuni ya Facebook Yazindua App Mpya ya Facebook Gaming

Ditty

Hii ni game ambayo binafsi yangu naipenda sana ni rahisi kucheza na ni nzuri sana. Game hii inakuwezesha kutuma sauti ikiwa kwenye mfumo wa muziki yani unauwezo wa kurecord sauti yako kisha unachagua moja kati ya sauti za nyimbo zilizopo kisha sauti yako inakua sambamba na nyimbo uliyo chagua kisha kumtumia yoyote kwenye facebook messenger, game hii ni nzuri sana na nirahisi kucheza pia unaweza uka save sauti hizo na kushare na watu hatakama hawatumi facebook messenger.

kwa wale wanaotumia iOS unaweza kupakua Application hiyo hapa chini.

[appstore id=957529556]

 

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.