in

Namna ya Kuondoa Password Kwenye iPhone Yoyote

Namna ya Kuondoa Password Kwenye iPhone Yoyote

Kama wote tunavyojua simu za iPhone pindi unapo sahau password yako hua ni mthiani sana kutumia simu yako wengi wetu hapa tanzania ukimbilia kuflash simu zao hivyo hupoteza pesa na muda pia, lakini kuna njia nyingi za kuondoa password uliyosahau kutoka kwenye kifaa chako cha apple bila kutumia gharama yoyote.

Vitu unavyoitaji ili kufanikisha kuondoa password kwenye simu yako ya iPhone ni vifuatavyo:

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  1. Waya original wa iPhone (hakikisha waya huo unauwezo wa ku-connect vizuri simu yako kwenye iTune)
  2. Computer yenye uwezo wa kawaida yenye window 7, 8, au 10.
  3. Hakikisha ume-download na ku-install application ya iTune kwenye computer yako Download Hapa

Ili uweze kufungua kifaa chako cha apple ni lazima kifaa chako kiwe ni iPhone, iPod touch au iPad, njia hizi zimesha fungua simu za iPhone 5, iPhone 4s, iPod Nano na iPad na nyingine, hiyo basi njia hii ni slama na ya uwakika na rahisi kufanya.

KUMBUKA: Kwa kufanya njia hii vitu vyote vilivyoko kwenye simu yako vitapotea kwa hiyo ni vema kama una soma hii na unatumia iPhone uwe na mtindo wa kupenda kufanya Back up ya simu yako kila mara.

MELEKEZO

  1. Shikilia vibonyezo vya Home+power kwa pamoja hakikisha mpaka umeona slide ya power off inakuja.
  2. Endelea kushikilia usiachie wala usibonyeze slide ya kuzima simu endelea kushikilia kwa seconde 10 baada ya kuona Slide ya power.
  3. Unapoona logo ya Apple ondoa kidole chako kwenye kibonyezo cha power, lakini endelea kushikilia kibonyezo cha Home.
  4. Endelea kushikilia mpaka uone simu yako imeandika Connect to iTune.
  5. Chomeka simu yako kwenye iTune kisha nenda kwenye menu zilizoko juu upande wa kushoto na restore simu yako.

Kwa kufanya njia hizi simu yako itakua imeondoa password na utaweza kutumia tena kama mwanzoni, kumbuka njia hii usababisha kufuta kila kitu kwenye simu yako kwa hiyo ni vema kuifadhi back up ya simu yako kabla ya kufanya njia hii. Kama njia hii haijafanya kazi kwenye simu yako usisite kutuandikia hapa Smartphone Help Center (namna ya kuliza swali ni rahisi join kwenye group subiri utakua approved alfu nenda kwenye poll kisha uliza swali lako) na tutakujibu haraka zaidi na kumbuka kufuatilia blog hii kwa njia nyingine zaidi.

Namna ya Kuondoa Password Kwenye iPhone Yoyote
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Fahamu Maana ya Alama Hizi Kwenye Vifaa vya Elektroniki

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

9 Comments