in

Application ya Telegram Yafikisha Watumiaji Milioni 100

Wengi wanoa tumia application ya Telegram utawasikia wakisema kuwa application hiyo ni nzuri sio kwa sababu ya watengenezaji wake, bali ni sababu application hiyo inaonyesha kuwa na baadhi ya vitu ambavyo application ya Whatsapp haina. Pia Application hiyo ya Telegram imeonekana kutumika kwenye simu za aina nyingi kuliko ile ya Whatsapp, Telegram inapatikana kwenye simu za aina nyingi wakati application ya Whatsapp inatumia zaidi Android na Apple.

Hivi karibuni application hiyo ilitoa twakimu za watumiaji na kuonyesha kuwa application hiyo ina watumiaji zaidi ya milioni 100 kila mwezi, idadi hiyo inaenda ikiongezeka kila siku pia application hiyo ina kuwa na watumiaji wapya karibia laki 350,000 kila siku. Hii inaonyesha kuwa application hii sasa inaonekana kutumiwa sana na watumiaji wa smartphone kote duniani, hata hivyo Telegram inapokea na kutuma message zisizo pungua bilioni 15 kila siku, katika mahesabu ya kawaida ni sawa na message 150 kwa kila mtumiaji.

Telegram
Price: Free

Kampuni ya Facebook Yazindua App Mpya ya Facebook Gaming
Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.