in

Letterboxd Social Media Kwaajili ya Wapenda Filamu

Letterboxd

Letterboxd ni website nzuri sana kama wewe ni mpenzi wa filamu, website hii inaunganisha wapenda filamu kote duniani kwa mfumo wa review yani mapitio website hii inaunganisha ni moja kati ya social media zinazokuwa kwa kasi kwani kwa sasa website hiyo ina watu zaidi ya milioni 10.

Hivi karibuni website hiyo imetoa application yake kwenye mfumo wa iOS, application hiyo inafanya kazi sawasawa na website yake lakini hii application ni rahisi zaidi. unachotakiwa kufanya ni kujiunga na kisha kuanza kuweka movie ulizowahi kuangalia kisha na kisha utoe maoni yako juu ya movie hizo. Pia application hii itakusaidia kujua movie mpya zinazotoka kila siku pamoja na kujua movie ipi ni nzuri kutokana na maoni ya watu walio wahi kuangalia movie hiyo, application hiyo pia itakusaidia kupata marafiki wapya wanaopenda movie kote duniani.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Application hii ni rahisi sana kutumia na ni nzuri sana kama wewe ni mpenda filamu kwa watumiaji wa android application hii haijafika kwa hiyo hii ni kwa wale wenye simu zenye mfumo wa iOS. Ila pia kama unatumia android unaweza kutembelea website yao hapa www.letterboxd.com kisha ujisajili na uanze kufurahia ulimwengu wa filamu.

Kwa wenye iOS unaweza kupakua Application Hiyo Hapa

‎Letterboxd
Price: Free+

 

Letterboxd Social Media Kwaajili ya Wapenda Filamu
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Hizi Hapa Browser Bora Zenye Mfumo wa Akili Bandia (AI)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.